Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:43

Marekani yasema ISIS ni hatari na tishio kubwa


Waziri wa Ulinzi Marekani, Chuck Hagel na Jenerali Martin Dempsey, Aug. 21, 2014
Waziri wa Ulinzi Marekani, Chuck Hagel na Jenerali Martin Dempsey, Aug. 21, 2014

Hagel aliwaambia waandishi habari kuwa kundi hilo la Islamic State halina utu wala uwajibikaji wowote unaoashiria hulka ya kibinadamu.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amesema kitisho cha kundi lenye msimamo mkali la Islamic State (ISIS) kwa usalama wa dunia ni zaidi ya kitu chochote tulichowahi kuona.

Hagel alikuwa akizungumza na waandishi habari Alhamis jijini Washington, ambapo aliwaelezea wanamgambo hao wa Iraq kuwa hatari zaidi ya makundi ya kigaidi tunayoyajua. Alisema limejipanga na kuratibisha dhana yake na mikakati yake ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kijeshi.

Waziri Hagel alisema kundi hilo lina ufadhili mzuri wa kifedha na ni tishio la hivi sasa kwa maslahi ya Marekani ndani na nje ya nchi.

Hagel aliwaambia waandishi habari kuwa kundi hilo la Islamic State halina chembe chembeya utu wala uwajibikaji wowote unaoashiria hulka ya kibinadamu.

Alitoa matamshi hayo siku chache baada ya wanamgambo hao wa ISIS kutoa ukanda wa video ukionyesha jinsi walivyomwua kwa kumkata kichwa mwandishi habari raia wa Marekani James Wright Foley.

Waziri huyo wa ulinzi alikuwa pamoja na mwanajeshi wa ngazi ya juu wa Marekani Jenerali Martin Dempsey, aliyelielezea kundi la Islamic State kuwa lenye maono sawa na yaliyobashiriwa kwenye vitabu vitakatifu kuhusu siku za mwisho duniani.

XS
SM
MD
LG