Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:38

Marekani yaridhishwa na maendeleo nchini Rwanda


Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch katika ziara yake nchini Rwanda.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch katika ziara yake nchini Rwanda.

Serikali ya Marekani imetangaza kuridhishwa na maendeleo ya sekta ya sheria nchini Rwanda na kuahidi kuendelea kushirikiana na nchi hiyo kupiga hatua zaidi. Mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani Loretta Lynch anayefanya ziara nchini Rwanda aliyasema hayo mjini Kigali huku akiendelea kukutana na viongozi wa serikali ya nchi hiyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:56 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kwa miaka 21 iliyopita Rwanda imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mataifa ya kigeni kwa kusuasua kuwaleta washukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda kwa madai kwamba mfumo wa sheria wa nchi hiyo ulikuwa na hitilafu.Lakini kadri ya miaka ilivyosogea ndivyo mtazamo huo ulivyoendelea kubadilika na kusababisha nchi za kigeni hasa Marekani na ulaya kuanza kuwarejesha Rwanda washukiwa wa mauaji ya Rwanda waliokamatwa kwenye mataifa hayo ili kesi zao ziweze kusikilizwa Rwanda.

Sasa Marekani imetangaza wazi kwamba iko tayari kuendelea kuisaidia Rwanda kutokana na nchi hiyo kupiga hatua ya kuridhisha kwenye mfumo wa sheria zake. Alisema mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani Loretta Lynch.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch
Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch

“Mabadiliko kama urahisishaji wa kutoa sheria, kuufanya mfumo mzima wa sheria kuwa rahisi kwa wanyarwanda wote na tumepata ufafanuzi mkubwa kuhusu ushirikiano baina yetu na naahidi kuendelea kushirikiana zaidi na serikali ya Rwanda”.

Hii imekuwa ni habari njema kwa serikali ya Rwanda kutokana na kupata uungwaji mkono kutoka kwa Marekani. Alisema waziri wa sheria na mwanasheria mkuu wa serikali ya Rwanda, Johnston Busingye, kwamba ilikuwa ni fursa kwa Rwanda kutoa rasilimali nyingine kwa ulimwengu. “Ni muhimu kwa ulimwengu mzima kuwafikisha kzimbani washukiwa wa mauaji ya kimbari, ni muhimu kwa ulimwengu kutambua kwamba kuna ulazima wa kufanya hivyo na hili tumezungumza kwa mapana na tumekubaliana pamoja juu ya hilo”.

Mwanasheria huyo mkuu wa serikali alisema kwamba ni lazima mfumo wa sheria uimarishwe kwa nchi mbalimbali kwa sababu sheria na haki ni vyombo muhimu katika kulifanya kila taifa kupiga hatua. Kiongozi huyo wa Marekani anafanya mazungumzo na viongozi wa Rwanda akiwemo Rais Paul Kagame.

Mapema Jumanne alizungumza kwenye kongamano la kimataifa la Interpol linaloendelea mjini Kigali ambapo aliyaomba mataifa ya ulimwengu kushirikiana kupiga vita biashara za kuuza watu ambazo alisema zimekithiri ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG