Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 14:43

Marekani yapiga marufuku uagizaji wa mafuta kutoka Rashia


Sehemu ya kiwanda cha mafuta kinachosimamiwa na kampuni ya mafuta, Lukoil kwenye bahari ya Baltic, Rashia. Septemba 16, 2021. Picha ya Reuters
Sehemu ya kiwanda cha mafuta kinachosimamiwa na kampuni ya mafuta, Lukoil kwenye bahari ya Baltic, Rashia. Septemba 16, 2021. Picha ya Reuters

Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne ametangaza marufuku ya kuagiza mafuta na bidhaa nyingine za nishati kutoka Rashia kama hatua ya kuiadhibu nchi hiyo kwa kuivamia Ukraine

“Tunapiga marufuku uagizaji wa mafuta yote na gesi kutoka Rashia, Biden amewambia waandishi wa habari kwenye Ikulu ya White House.

“Hiyo ina maana kwamba mafuta ya Rashia hatayakubaliwa tena katika bandari za Marekani”.

Rashia ni muazaji mkubwa wa mafuta na gesi ulimwenguni. Iliwekewa vikwazo vya kifedha duniani kutokana na vita vya Ukraine, lakini hadi sasa mauzo yake ya nishati yalikuwa yamesamehewa.

XS
SM
MD
LG