Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:19

Marekani yaonya kuwepo kwa mzozo mkubwa wa chakula Sudan.


Susan Rice, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa mataifa akiongea na waandishi wa habari baada ya baraza la usalama kukutana kuzungumzia suala la Sudan.
Susan Rice, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa mataifa akiongea na waandishi wa habari baada ya baraza la usalama kukutana kuzungumzia suala la Sudan.

Marekani inashutumu Sudan kwa kuzuia mashirika ya misaada kutokuingia katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

Marekani inaonya kuwepo kwa mzozo mkubwa wa chakula katika sehemu mbili za sudan, jambo ambalo haraka limepingwa na serikali ya sudan.

Onyo la Marekani lipo katika barua ambayo voa imeipata iliyosambazwa kwa wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa.

Barua inashutumu Sudan kwa kwa kuzuia mashirika ya misaada kutokuingia katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile, ambako serikali imekuwa ikipambana na makundi ya waasi tangu kati kati ya mwaka jana.

Balozi Rice alisema juhudi zimefanywa kuisihi serikali ya Sudan kutoa ruhusa ya kufikiwa maeneo yaliyoathiriwa, lakini licha ya mazungmzo, hakuna kilicho tendeka.

Lakini balozi wa Sudan katika umoja mataifa, Daffa Alla Elhag Osman, alilipinga onyo la balozi Rice la kutokea kwa mzozo wa chakula, akisema kuwa takriban asilimia 99 ya majimbo ya Blue Nile na Kordofan kusini yako katika hali kawaida.

XS
SM
MD
LG