Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:17
VOA Direct Packages

Marekani yaongeza msaada wa kijeshi kwa Somalia kwenye vita dhidi ya ugaidi


Wapiganaji wa al Shabab kwenye picha ya awali.
Wapiganaji wa al Shabab kwenye picha ya awali.

Marekani imeongeza msaada wake wa kijeshi kwa Somalia wakati taifa hilo likipiga hatua katika kukabiliana na mtandao wa kigaidi wa al Qaida ilioutaja kuwa mbaya zaidi ulimwenguni.

Marekani imeongeza msaada wake wa kijeshi kwa Somalia wakati taifa hilo likipiga hatua katika kukabiliana na mtandao wa kigaidi wa al Qaida ilioutaja kuwa mbaya zaidi ulimwenguni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, tani 61 za zilaha zimewasili kwenye mji mkuu wa Mogadishu Jumanne, ambazo Marekani kupitia taarifa imesema kwamba ni za kusaidia kwenye vita vya kihistoria vinavyoongozwa na jeshi la Somalia, dhidi ya wanamgambo wa al Shabab, likiwa limekomboa darzeni ya vijiji kutoka mikononi mwao tangu Agosti mwaka jana.

Kwenye taarifa tofauti ya pamoja, washirika wengine wakuu wa usalama: Qatar, Uturuki, UAE na Uingereza, pia wamesema kwamba watasaidia kwenye juhudi za Somalia za kidhibiti silaha, hatua itakayopelekea baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo vya kutouziwa silaha kwa taifa hilo. Mshauri wa kitaifa wa Somalia kwenye masuala ya usalama Hussen Sheikh Ali amesema kwamba walikuwa na mkutano wa kufana kupitia ujumbe wa twitter, muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao mjini Washington DC.

Mwaka uliopita, serikali ya Somalia chini ya rais Hassan Sheikh Mohamud ilitangaza vita dhidi ya maelfu ya wanamgambo wa al Shabab ambao kwa miongo kadhaa wamedhibiti maeneo kadhaa na kufanya mashambulizi mabaya, wakati wakitumia migawanyiko iliyopo baina ya koo na kujipatia mamilioni ya dola kila mwaka wakijitahidi kubuni taifa la kiislamu.

XS
SM
MD
LG