Desemba mwaka jana baraza la waakilishi lilitoa idhini kwa wizara hiyo ya kuelekeza mapato kutokana na mali za Russia zilizoshikiliwa, kwenye ukarabati wa Ukraine. Hata hivyo idhini hiyo ni kwa mali zilizoshikiliwa kuhusiana na ukiukwaji wa vikwazo vya Marekani chini ya amri maalum za kiutendaji za rais.
Kutokana na hilo, mamilioni ya dola kutokana na mali za Russia zilizoshikiliwa kutokana na kukiuka amri ya upelekaji nje wa bidhaa, pamoja na hujuma nyingine za kiuchumi haziwezi kutumika kwa ajili ya Ukraine. Sasa hivi wizara ya sheria ya Marekani inaomba bunge liongeze wigo wa mali zinazoweza kutumika kwenye ukarabati wa Ukraine.
Tangu uvamizi wa Russia wa Ukraine Februari mwaka jana, wizara ya sheria ikiongozwa na mkuu wa sheria Jenerali Merrick Garland imetwaa mali za mabwenyenye wa Russia, huku pia ikiendelea na uchunguzi wa uhalifu wa kivita dhidi yao.