Rais Joe Biden anasafiri kuelekea Philadelphia kujitolea katika taasisi ya misaada ya kuwasaidia wanaokabiliwa na njaa.
Huko South Carolina, Makamu wa Rais Kamala Harris anatarajiwa kutoa hotuba ambayo White House inaeleza itawashawishi watu “kutumia sauti zao kuendeleza mapambano ya haki na dhidi ya mashambulizi kwa misingi ya uhuru.
Shirika la serikali ya Marekani AmeriCorps ni moja ya jumuiya zilizojikita katika kutoa huduma zilizoandaa shughuli mbalimbali kwa ajili ya Siku ya Martin Luther King Jr ya Kujitolea Kitaifa huku watu kote nchini wakiitumia sikukuu hiyo kushiriki katika miradi ya huduma za jamii.
Kila mwaka katika Jumatatu ya tatu ya mwezi wa Januari, Wamarekani humuenzi King, kiongozi wa haki za kiraia ambaye katika miaka ya 1950 na 1960 aliandaa maandamano amani dhidi ya ubaguzi upande wa kusini, harakati za kutafuta usawa wa watu Weusi na haki zao za kupiga kura.
Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na shirika la habari la AP.
Forum