Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:50

Marekani yalaani mashambulizi ya Somalia.

Vikosi vya usalama vya Somalia na raia wakiwa nje ya hoteli ya Weheliye baada ya shambulizi la kigaidi.
Vikosi vya usalama vya Somalia na raia wakiwa nje ya hoteli ya Weheliye baada ya shambulizi la kigaidi.

Mashambulizi ya makombora pia yalisikika Ijumaa katika uwanja mkubwa wa mpira wa miguu wa zamani huko Mogadishu ambao sasa unatumika kama kambi kubwa ya umoja wa afrika.

Marekani imesema inashutumu vikali shambulizi la hivi karibuni la al- shaabab katika hoteli mbili na kambi la jeshi la umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

Takriban watu 16 wameuwawa katika mashambulizi hayo kwenye hoteli za Waheliye na Siyad ijumaa iliyopita.

Mashambulizi ya makombora pia yalisikika Ijumaa katika uwanja mkubwa wa mpira wa miguu wa zamani huko Mogadishu ambao sasa unatumika kama kambi kubwa ya umoja wa afrika.

hakuna majeruhi walioripotiwa kutokana na shambulizi hilo.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani jumapili ilisema al- shabab kwa mara nyingine imeonesha ukatili na kuikataa jumuiya ya Somalia kuondokana na ghasia na ukandamizaji.

XS
SM
MD
LG