Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 20:26

Marekani yakosoa Pakistan kwa kumkamata daktari


Marekani yakosoa Pakistan kwa kumkamata daktari

Daktari aliyesaidia kukamatwa kwa Bin Laden atiwa mbaroni

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya daktari wa Pakistan aliyesaidia Marekani kumpata kiongozi wa kundi la kigaidi Osama Bin Laden. Waziri Panetta alisema katika kipindi cha 60 Minutes cha kituo cha televisheni cha CBS kwamba Dr. Shikal Afridi alitoa habari za kijasusi zilizosaidia majeshi ya Marekani kumkamata na kumwua gaidi Osama Bin Laden tarehe 2 mwezi Mei mwaka jana katika mji wa Abbottabad. Mahojiano na waziri huyo wa ulinzi yatapeperushwa hewani Jumapili. Pakistan imemkamata Dr. Afridi na kumshtaki kwa kosa la uhaini. Daktari huyo aliyekuwa akifanyia marekani kazi za kijasusi, aliongoza program ya utoaji chanjo ili kupata DNA iliyothibitisha kuwepo kwa Bin Laden katika uwanja aliokutwa na kuuliwa huko Abbottabad. Bwana Panetta amesema hatua ya Pakistan ya kumkamata mtu aliyesaidia kumnasa gaidi kama huyo ni makosa makubwa. Waziri huyo wa ulinzi wa Marekani amesema anaamini kuwa kuna mtu katika mamlaka ya Pakistan aliyejua fika mahali Bin Laden alikuwa akijificha.

XS
SM
MD
LG