Margaret Taylor, mshauri wa sheria wa wizara ya mambo ya nje anayeiwakilisha Marekani, Jumatano ametoa hoja kwamba mahakama ya ICJ si sehemu sahihi kushughulikia masuala ya haki za masuala ya hali ya hewa.
Amesema idara ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya hali ya hewa na mkataba wa Paris ni majukwaa pekee ya kimataifa kisheria ambayo yapo mahsusi yaliyowekwa na mataifa kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana lilitoa mwito kwa mahakama ya ICJ kuzungumzia kisheria kama mataifa yanayo changia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuwajibishwa kisheria kwa kusababisha tatizo hilo na madhara inayoleta.
Forum