Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:45

Marekani yaiondoa rasmi Sudan katika orodha ya ugaidi


Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok.

Ubalozi wa Marekani mjini Khartoum Jumatatu umesema Rais Donald Trump ameiondoa rasmi Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani.

Hatua hiyo itapelekea taifa hilo kupata mikopo ya kimataifa ili kufufua uchumi wake uliodidimia.

Ubalozi wa Marekani umeandika kwenye ukurusa wake wa Facebook kwamba hatua hiyo inaanza kutekelezwa rasmi leo jumatatu, na kwamba taarifa iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo itachapishwa kwenye gazeti la serikali kuu.

Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo
Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo

Sudan ilitajwa kama taifa linalofadhili ugaidi miaka ya 1990 wakati nchi hiyo ilipompa hifadhi ya muda mfupi aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden na wanamgambo wengine wa kundi hilo ambao walikuwa wanatafutwa.

Sudan iliaminika pia ilikuwa njia inayotumiwa na Iran kwa kupeleka silaha kwa wanamgambo wa Palestina katika ukanda wa Gaza.

Hatua hiyo ya Marekani ilikuwa ni kichocheo kikubwa kwa serikali ya Khartoum kurejesha uhusiano wake na Israel.

Nchi hizo mbili zilikuabaliana kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia, na kufanya Sudan kuwa taifa la tatu la kiarabu kurejesha uhusiano na Israel baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain.

XS
SM
MD
LG