Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:35

Marekani yageuza ukurasa wake  juu ya vizuizi vya uhamiaji vilivyo kuwepo enzi ya janga la corona


Wahamiaji wamekusanyika kwenye mpaka wa Marekani na Mexico baada ya kuondolewa sheria ijulikanayo kama Title 42. REUTERS.
Wahamiaji wamekusanyika kwenye mpaka wa Marekani na Mexico baada ya kuondolewa sheria ijulikanayo kama Title 42. REUTERS.

Marekani iligeuza ukurasa wake  juu ya vizuizi vya uhamiaji vilivyo kuwepo enzi ya janga la corona huku kukiwa na utulivu katika mpaka wake na Mexico wakati wahamiaji walikubaliana na kanuni mpya zinazolenga kutoshawishi uvukaji haramu .

Marekani iligeuza ukurasa wake juu ya vizuizi vya uhamiaji vilivyo kuwepo enzi ya janga la corona huku kukiwa na utulivu katika mpaka wake na Mexico wakati wahamiaji walikubaliana na kanuni mpya zinazolenga kutoshawishi uvukaji haramu na wasubiri ahadi ya njia mpya za kisheria za kuingia nchini Marekani.

Siku nzima baada ya kanuni iliyojulikana kama Title 42 kuondolewa, wahamiaji na maafisa wa serikali siku ya Ijumaa walikuwa bado wanatathmini athari za kutumia kanuni mpya zilizopitishwa na utawala wa Rais Joe Biden kwa matumaini ya kuleta utulivu katika eneo la mpaka wa Kusini-magharibi na kupunguza wasafirishaji wa magendo wanaowatoza fedha wahamiaji kufika huko.

Wahamiaji sasa kimsingi wamezuiliwa kutafuta hifadhi nchini Marekani ikiwa hawakuomba kwanza mtandaoni au kutafuta ulinzi katika nchi walizopitia. Familia zinazoruhusiwa kuingia wakati kesi zao za uhamiaji zikiendelea zitakabiliwa na marufuku ya kutotoka nje na kuwepo kwa ufuatiliaji wa GPS.

Na kwa wale waliofukuzwa Marekani, sasa wanaweza kuzuiliwa kuingia nchini kwa miaka mitano na kukabiliwa na mashtaka ya jinai

XS
SM
MD
LG