Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:03

Marekani yaelezea wasi wasi kuhusu uchaguzi Uganda


Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati akifanya kampeni nchini humo
Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati akifanya kampeni nchini humo

Serikali ya Marekani imeelezea wasi wasi wake kuhusu uamuzi wa serikali ya Uganda kuzuia mitandao kadhaa ya kijamii na vituo vidogo vya fedha kuanzia siku ya uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamis Februari 18 na kumsihi Rais wa Uganda Yoweri Museveni kusitisha mara moja hatua hiyo.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry alipozungumza kwa njia ya simu Ijumaa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisisitiza kwamba maendeleo ya Uganda yanategemea majukumu ya mtu kufuata kanuni za kidemokrasia katika utaratibu unaoendelea wa uchaguzi na kwamba Marekani inasimama na watu wa Uganda wakati wanapotumia demokrasia hii muhimu.

Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye
Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye

Waziri Kerry pia alielezea wasi wasi wake kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Kizza Bessigye na kusumbuliwa kwa wafuasi wa chama cha upinzani wakati wa upigaji kura na mikutano ya kisiasa na alitoa wito kwa Rais Museveni kutoa muongozo sahihi kwa polisi na vikosi vya usalama akieleza kwamba hatua kama hizo zinazofanywa na polisi zinachangia kujiuliza majukumu ya Uganda katika kufanikisha utaratibu wa uchaguzi ulio huru, wazi na wenye hadhi bila kuwepo manyanyaso.

Katika mazungumzo hayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alielezea suala la ucheleweshwaji wa kufunguliwa vituo vya kupiga kura. Aliendelea kusema kwamba alitiwa moyo na tume ya uchaguzi kuchukua hatua za kuongeza muda wa kupiga kura kwa maeneo kadhaa ambayo hayakufunguliwa kwa wakati.

XS
SM
MD
LG