Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 23:13

Marekani yasikitishwa na kasoro za uchaguzi Rwanda


Taarifa ya Marekani pia ilisifia vyombo vya habari Rwanda kuripoti malalamiko ya bugudha zinazotokea kwa baadhi ya wagombea wa upinzani

Marekani ilisema Jumamosi kwamba ilisikitishwa na kasoro zilizoonekana wakati wa upigaji kura katika uchaguzi wa Rwanda ambapo Rais wa muda mrefu Paul Kagame alishinda kwa takribani asilimia 99 ya kura.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press ni kwamba taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilielezea wasi wasi mkubwa juu ya utaratibu katika upigaji kura. Kagame alishinda kirahisi muhula wa tatu madarakani katika kile alichokiita utaratibu unaofanyika siku ya kupiga kura. Anatarajiwa kuongoza miaka saba mingine katika taifa hilo dogo lililopo Afrika mashariki akisifiwa kwa kazi yake nzuri ya kuinua uchumi wa nchi hiyo lakini pia akikosolewa kwa kuwanyamazisha wapinzani wake.

Paul kagame
Paul kagame

Maafisa wa uchaguzi walisema bwana Kagame alishinda asilimia 98.63 ya kura. Wapinzani wake wote wawili hakuna yeyote aliyeshinda point nyingi za kukaribia ushindi kamili. Taarifa ya Marekani pia ilisema inaendelea kuwa na wasiwasi kutokana na kutokuwepo uwazi katika kuelezea mitazamo ya wagombea wengine na pia ilisifia vyombo vya habari vya Rwanda kwa kuripoti malalamiko ya bugudha zinazotokea kwa baadhi ya wagombea wa upinzani.

Kagame alikabiliwa na changamoto kutoka kwa wagombea wawili wa upinzani katika kiti cha urais huku wagombea watatu wengine wa kinyang’anyiro hicho cha urais walishindwa kuendelea na azma yao kutokana na kutofikia sifa za viwango vilivyohitajika kuwania nafasi hiyo, ikiwemo kupata sahihi za kutosha za uidhinishwaji kama mgombea urais.

XS
SM
MD
LG