Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:50

Marekani yadai kuwa na chanjo za kutosha za Covid


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Wakati kukiwa na zaidi ya dozi milioni 40 za ziada za corona, maafisa wa afya wa Marekani wanasema kwamba zitatosha wakongwe wanaohitaji chanjo ya tatu maarufu kama booster pamoja na watoto wadogo amabo chanjo zao zinatarajiwa kuidhinishwa hivi karibuni. 

Idadi ya watu wanaohitaji chanjo inatarajiwa kuongeza maradufu wiki hii kufuatia tangazo la serikali la wiki iliyopita, la kuindhinisha utoaji wa chanjo za booster.

Licha ya juhudi za serikali za kurai watu kupokea chanjo, kwa kuwaahidi zawadi za aina mbalimbali, bado kuna watu takriban milioni 70 ambao hawajapokea chanjo zao. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, idadi ya vifo vya kila siku hapa Marekani kutokana na corona imepanda hadi zaidi ya 1,900 katika wiki za karibuni.

Utengenezaji madhubuti wa chanjo hapa Marekani umepelekea rais Joe Biden kuahidi msaada wa dozi milioni 500 aina ya Pfizer kwa mataifa ya kigeni. Makundi ya kutoa misaada yamekuwa yakishinikiza Marekani pamoja na mataifa mengine yenye uwezo kutoa chanjo kwenye mataifa maskini ambayo, baadhi hayajapokea hata chanjo za kwanza kwa watu wake.

Maafisa wameongeza kusema kwamba baadhi ya majimbo hapa Marekani yamekuwa yakiagiza dozi nyingi zaidi ya zinazohitajika na kwa hivyo kupelekea kuharibika kwake.

XS
SM
MD
LG