Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:48

Marekani yaangalia uwezekano kufungua vituo zaidi vya kijeshi Afrika


Kikosi maalumu cha jeshi la Marekani katika juhudi za kusaidia ugaidi barani Afrika
Kikosi maalumu cha jeshi la Marekani katika juhudi za kusaidia ugaidi barani Afrika

Jeshi la Marekani linaangalia uwezekano wa kufungua maeneo 11 ya kituo cha pili barani Afrika kwa mujibu wa msemaji wa AFRICOM. Kanali Mark Cheadle, alizungumza na sauti ya Amerika- VOA mjini Brussels hapo Jumanne lakini hakuelezea maeneo yapi jeshi linafikiria uwezekano wa kuwa na kituo cha pili, zaidi ya kuelezea kwamba Nigeria sio mojawapo.

Marekani kwa sasa ina kituo kimoja cha kijeshi katika taifa la Djibouti huko Afrika ya mashariki. Vikosi vya Marekani pia vipo nchi kavu nchini Somalia ili kusaidia mapigano ya kieneo dhidi ya kundi la wanamgambo wa al-Shabaab na nchini Cameroon ili kusaidia juhudi za mataifa mbali mbali kupambana dhidi ya kundi la Boko Haram lenye makao yake nchini Nigeria.

Kamanda wa AFRICOM, Jeneral David Rodriguez
Kamanda wa AFRICOM, Jeneral David Rodriguez

Kamanda wa AFRICOM, Jenerali David Rodriguez aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kwamba jeshi la Marekani liliwapa mafunzo wanajeshi wa kikosi cha ki-intelijensia cha Nigeria pamoja na wanajeshi watatu wa mapigano huko Nigeria akiwemo mmoja ambaye ndio kwanza amehitimu.

XS
SM
MD
LG