Licha ya kuhudumu kwa muda mfupi zaidi kuliko kiongozi yeyote wa Marekani, Kennedy aliyekuwa na umri mdogo wakati huo pamoja na mke wake Jacqueline, walibadili namna mambo yanavyoendeshwa kwenye ofisi ya rais ya Marekani.
Utawala wa Kennedy ulishinikiza Marekani kujikwamua kutokana na athari za vita, na badala yake kukumbatia nafasi zilizokuwemo, pamoja na ubunifu. Wakati wa kuapishwa kwake Januari 1961, Kennedy alisema, “Usiulize unachoweza kupata kutoka kwa nchi yako, bali jiulize unachoweza kuifanyia nchi yako.”
Wakati wa kilele cha vita baridi na Muungano wa Sovieti, Kennedy alitumia uwezo wake wote, kuhimiza uwezo na ushawishi wa kidiplomasia wa Marekani kote ulimwenguni.
Forum