Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 16:58

Marekani, Uturuki waendelea na ulinzi wa doria ya pamoja Syria


Askari wa Uturuki wakifanya doria katika mpaka wa Syria Julai 24, 2015.

Ushirikiano kati ya Marekani na Uturuki unaendelea kuimarika Syria, pamoja na kuwepo mgogoro wa mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa Jeshi la Uturuki, nchi hizo mbili ambazo ni washirika wa Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO) wana karibia kuanza kufanya ulinzi wa doria ya kijeshi wa pamoja katika mkoa wa Manbij kaskazini mwa Syria.

“Ingawaje zoezi hilo limechelewa kwa siku chache kwa mujibu wa ratiba, mpangilio huo unaendelea bila ya kizuizi chochote.

Hivi sasa tunaanza kipindi cha ulinzi wa doria ya pamoja,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amewaabia waandishi Jumapili.

Manbij imeendelea kuwa ni sehemu yenye mvutano katika mahusiano yaliyoko kati ya Marekani na Uturuki tangu wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF) walipouteka mji huo uliokuwa mikononi mwa kikundi cha Islamic State.

Sehemu kubwa ya kikundi cha SDF kinawapiganaji wa kikundi cha wanamgambo wa Kikurdi wa Syria, na kikundi cha YPG ambacho kimetajwa kuwa ni magaidi na Ankara kikiwa na mafungamano na chama cha PKK. Washington na Umoja wa Ulaya umekitaja kikundi cha PKK kuwa ni jumuiya ya magaidi.

Msaada wa kijeshi unaotolewa na Washington kwa kikundi cha YPG katika vita yake dhidi ya kikundi cha Islamic State ikiwa ni sababu kuu ya mgogoro unaoongezeka na Ankara.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG