Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:32

Marekani yatangaza kwamba Russia haina haki ya majibu ya kulipiza kisasi


Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Heather Nauert.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Heather Nauert.

Marekani imetangaza alhamisi kwamba Russia haina haki ya majibu ya kulipiza kisasi ya kuwafukuza wanadiplomasia wa Marekani.

Baadaye siku hiyo Marekani ilisema hatua hiyo ya Russia inaendelea kudumaza uhusiano kati yao na Marekani.

Kuondolewa kwa maafisa wa ujasusi wasiotangazwa wa Russia na Marekani na zaidi ya dazeni mbili ya nchi washirika pamoja na NATO mapema wiki hii ilikuwa ndio hatua sahihi ya kujibu shambulizi la kemikali la Russia kwenye ardhi ya Uingereza .Majibu ya Russia hayakutarajiwa na Marekani itapambana nao taarifa hiyo ilieleza..

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Heather Nauert, pia alikosoa hatua za Moscow zilizotangazwa mapema siku hiyo na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Sergey Lavrov.

XS
SM
MD
LG