"Tunazungumza juu ya bei ya kikomo au bei maalum ambayo itadumisha na kuimarisha vikwazo vya hivi karibuni vya nishati vilivyopendekezwa na Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza na wengine, ambayo itateremsha bei ya mafuta ya Russia na kupunguza mapato ya Putin, huku ikiruhusu usambazaji zaidi wa mafuta kufika kwenye soko la kimataifa," Yellen amewambia waandishi wa habari mjini Toronto.
"Tunadhani bei maalum pia ni njia muhimu ya kuzuia madhara mabaya kwa nchi maskini zenye pato la chini ambazo zinataabika kutokana na gharama ya juu ya chakula na nishati," Yellen amesema, akizungumza pamoja na waziri wa fedha wa Canada Chrystia Freeland.