Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:47

Marekani na Uturuki zataka Assad ang'atuke


Rais Barack Obama na waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika White House, Mei 16, 2013.
Rais Barack Obama na waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika White House, Mei 16, 2013.

Rais Obama alisema kuwa wote wanakubali kwamba Assad lazima aondoke. Na kwamba anapaswa kukabidhi madaraka kwa viongozi wa serikali ya mpito.

Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamesema wataendelea kushinikiza rais wa Syria Bashar al-Assad aondoke madarakani.

Katika mkutano wa pamoja kutoka White House, viongozi hao wawili walipuuzilia tofauti zao juu ya Syria na badala yake wakasisitiza umuhimu wa kuiwekea shinikizo serikali ya Assad huku wakiendelea kusaidia makundi ya upinzani nchini humo.

Rais Obama alimtambua Bw. Erdogan kwa kuwa mbele katika juhudi za kupatikana kwa Syria yenye demokrasia na kusema kuwa Uturuki itakuwa na jukumu kubwa katika wiki zijazo.

Rais Obama alisema kuwa wote wanakubali kwamba Assad lazima aondoke.Na kwamba anapaswa kukabidhi madaraka kwa viongozi wa serikali ya mpito.

Mkutano huo wa Alhamis baina ya viongozi hao wawili, pia ulijadili mazungumzo ya kurejesha uhusiano mwema baina ya Israel na Uturuki. Bw. Erdogan anasema ana mipango ya kuzuru Gaza na Ukingo wa Magharibi hapo Juni.
XS
SM
MD
LG