Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:18

Marekani na Ufaransa zataka jeshi la Afrika nchini Mali


Wapiganaji wa kundi moja la ki-Islam la MUJAO wakiwa karibu na uwanja wa ndege wa Gao, Mali.
Wapiganaji wa kundi moja la ki-Islam la MUJAO wakiwa karibu na uwanja wa ndege wa Gao, Mali.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema wakati umefika kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha jeshi linalo-ongozwa na Afrika kwa Mali.

Marekani na Ufaransa wanaitaka Umoja wa Mataifa kuunga mkono jeshi la ulinzi wa amani linaloongozwa na Afrika kurejesha amani kaskazini mwa Mali ambako wanamgambo waasi wa Tuareg na magaidi wenye uhusiano na al-Qaida wamepanua udhibiti wao tangu mapinduzi ya mwezi Machi dhidi ya serikali ya kiraia huko Bamako.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande anasema wakati umefika kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha jeshi linalo-ongozwa na Afrika kwa Mali.

Rais Hollande anasema jeshi chini ya Umoja wa Afrika na jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi-ECOWAS litasaidia kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel na kuisaidia Mali kulipanga tena jeshi lake ili kukabiliana na vitisho vya baadaye.

Hollande alizungumza kwenye mkutano uliofanyika pembeni ya kikao cha mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa huko new York nchini Marekani. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliuambia mkutano huo kwamba machafuko na ghasia nchini Mali zinatishia uthabiti kote katika eneo huku hatari ikikua zaidi ya kile anachokiita makundi yenye sera kali yanayotaka kuleta itikadi za kikatili.

Hivyo basi waziri Clinton anasema ni wakati kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kuliunga mkono jeshi linalopambana katika eneo hilo.
XS
SM
MD
LG