Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:15

Marekani na Saudia waaunga mkono maeneo salama, Syria na Yemen


Rais Trump akizungumza na mfalme wa Saudia, Salman
Rais Trump akizungumza na mfalme wa Saudia, Salman

Ikulu ya Marekani-White House ilisema Rais Donald Trump na mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abd al-Aziz Al Saud walikubaliana kuunga mkono maeneo salama huko Syria na Yemen.

Viongozi hao wawili walizungumza kwa njia ya simu Jumapili wakihakikishiana kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Marekani na Saudi Arabia. Taarifa ya White House ilisema Trump alimomba mfalme kusaidia maeneo salama na mfalme alikubali. Pia walisema watasaidia kile White House inachokiita mawazo mengine kusaidia wakimbizi wanaokimbia kutoka kwenye nyumba zao kwa sababu ya vita na umuhimu wa kutekelezwa kikamilifu mkataba wa nyuklia na Iran ambao Rais Trump anaukosoa kama ni mkataba mbaya.

Katika muda wa siku mbili zilizopita Rais Trump amekua akizungumza kwa njia ya simu na viongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Korea kusini na Japan pamoja na viongozi wa ulaya mwishoni mwa wiki.

XS
SM
MD
LG