Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:16

Marekani na Misri zatafuta njia mpya kupata amani mashariki ya kati


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (L) na Rais wa Misri, Abdel-Fattah el-Sissi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (L) na Rais wa Misri, Abdel-Fattah el-Sissi.

Marekani na Misri siku ya Jumatano walitafuta njia za kufufua utaratibu wa mazungumzo ya amani kati ya Israel na wapalestina baada ya Rais wa Misri Abdel-fattah el-Sissi kusema wiki hii kwamba atafanya juhudi zote ziwezekanazo kupata suluhisho.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alikutana na kiongozi wa Misri mjini Cairo ambapo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani baadae alisema mwanadiplomasia huyo wa cheo cha juu wa Marekani alielezea shukrani zake kwa uungaji mkono thabiti wa el-Sissi katika kusonga mbele amani kati ya wa-Arabu na Israel.

Lakini msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mark Toner, hakuelezea kwa kina juu ya juhudi zozote mpya za kufufua tena utaratibu wa mazungumzo ya amani kati ya Israel na wa-Palestina ambayo yalivunjika kwama 2014 bila ya makubaliano.

Mkutano wa bwana Kerry na bwana el-Sissi umekuja siku moja baada ya kiongozi huyo wa Misri kusema mkataba wa Israel na wa-Palestina utafanya mahusiano ya Cairo na Tel Aviv kuwa ya mwamko.

XS
SM
MD
LG