Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:53

Marekani na Japan zinaanza hatua kuzuia vitisho vya China


Waziri wa ulinzi wa marekani, Lloyd Austin
Waziri wa ulinzi wa marekani, Lloyd Austin

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin wanafanya mkutano Jumatano unaoitwa 2+2 mjini Washington na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Hayashi Yoshimasa pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Japan Hamada Yasukazu

Marekani na Japan zitaelezea leo Jumatano hatua za kuzuia kuongezeka kwa vitisho vya kijeshi vya China katika East China Sea na eneo karibu na Taiwan, ikiwa ni pamoja na mipango ya kupanga upya vitengo vya Jeshi la Wanamaji la Marekani vilivyoko Okinawa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin wanafanya mkutano Jumatano unaoitwa 2+2 mjini Washington na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Hayashi Yoshimasa pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Japan Hamada Yasukazu.

Afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema Marekani na Japan zitatoa taarifa ya pamoja ambayo inaelezea "hatua za majibu" huku kukiwa na ongezeko la vitisho vya usalama kutoka Jamhuri ya Watu wa China.

"Changamoto kubwa ni China, ambayo katika kipindi cha miaka 15 hadi 20 iliyopita imeimarisha tabia yake ya kubembeleza, sio tu katika South China Sea, sio tu katika maeneo ya mpakani mwa nchi jirani, lakini pia katika East China Sea, karibu na Senkaku na karibu na Taiwan," alisema afisa huyo ambaye aliwaeleza waandishi wa habari juu ya historia hiyo.

XS
SM
MD
LG