Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Agosti 20, 2022 Local time: 02:34

Marekani: Mwanaume aliyembaka binti wa miaka 10 akamatwa na kushtakiwa


Wanawake wanaotetea haki ya kutoa mimba waandamana mbele ya nyumba ya jaji wa mahakama ya juu ya Marekani, mjini Alexandria, May 9, 2022. Picha ya AFP

Mwanaume mmoja wa jimbo la Ohio hapa Marekani ameshtakiwa kwa kumbaka binti wa miaka 10 ambaye alilazimika kusafiri hadi jimbo jirani la Indiana kutoa mimba.

Rais Joe Biden hivi karibuni alizungumzia kisa hicho akidhihirisha hasira yake juu ya uamuzi wa mahakama ya juu ya Marekani kubatilisha haki ya kutoa mimba nchini kote.

Gerson Fuentes alikamatwa Jumanne, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, na kufikishwa mahakamani Jumatano katika kaunti ya Franklin, mahakama ya wilaya.

Polisi wamesema, inaonekana Fuentes, mwenye umri wa miaka 27 alikuwa anaishi nchini Marekani kinyume cha sheria, na alikiri kumbaka msichana huyo mara mbili, mchunguzi wa polisi ametoa ushahidi mahakamani.

Fuentes anashikiliwa kwa dhamana ya dola milioni 2 na atasikilizwa katika kesi ya awali Julai 22.

Muathiriwa alifanyiwa operesheni ya kutoa mimba mjini Indianapolis tarehe 30 Juni, kulingana na ushahidi wa afisa huyo wa polisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG