Katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa mji huo, Meya Philp Jones amesema kwamba ni vigumu sana kuelewa kwamba mtoto mwenye umri wa miaka 6 alibeba bunduki kwenda nayo shule na kumpiga mwalimu risasi.
Hata hivyo amesema kwamba tukio hilo ni kuonyesha hali ambayo inaendelea Marekani.
Tukio la mtoto mwenye umri wa miaka 6 kumpiga risasi mwalimu lilitokea katika shule ya msingi ya Richneck.
majina ya mwalimu na ya mtoto huyo hayajatolewa na polisi.
Mtoto huyo anazuiliwa na polisi ambao wamesema kwamba tukio hilo halikuwa ajali na haijulikani namna mtoto alivyopata bunduki.
Facebook Forum