Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:43

Marekani: Mafanikio ya amani kwa mashariki ya kati bado yapo mbali


دُبئ ایئر شو میں متحدہ عرب امارات کی ایئر فورس کی ایروبیٹک ٹیم نے شاندار مظاہرہ پیش کیا
دُبئ ایئر شو میں متحدہ عرب امارات کی ایئر فورس کی ایروبیٹک ٹیم نے شاندار مظاہرہ پیش کیا

Rais wa Marekani Barack Obama aliwaeleza viongozi wa Israel na Palestina hakutakuwa na mafanikio yeyote kuelekea amani itakapofika muda wake wa kuondoka madarakani hapo mwanzoni mwa mwaka 2017, kwa mujibu wa maafisa wa White House.

Taarifa imekuja wakati bwana Obama anajiandaa kuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu huko White House siku ya Jumatatu.

Rais Barack Obama (R) na Waziri Mkuu wa Israel, Netanyahu
Rais Barack Obama (R) na Waziri Mkuu wa Israel, Netanyahu

Mkutano huo unaonekana kama juhudi ya kurekebisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa muda mrefu wa kijeshi wa Marekani na serikali ya Israel ambayo inapinga vikali mkataba wa nyuklia wa Iran.

Bwana Obama pia atautumia mkutano huo kumshinikiza bwana Netanyahu kuelezea kwa kina sera zake kwa wapalestina, kwa mujibu wa Rob Malley, ofisa wa baraza la usalama wa taifa kwa mashariki ya kati huko White House.

Bwana Rob alisema kwamba Rais Obama alisema tunatakiwa kufikia tathmini ya kweli ambapo hakutakuwa na mkataba wa kina wa mwisho katika kipindi kilichobaki cha muhula wake madarakani na pengine huwenda hakutakuwa na mashauriano muhimu kati ya pande hizo mbili.

“Ukichukulia ukweli huo, ambapo ni jambo jipya, waziri mkuu mwenyewe anaiona israel inavyosonga mbele”? Alihoji Malley.

Rais Barack Obama (R) na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas
Rais Barack Obama (R) na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas

Utawala wa Rais Obama umefanya juhudi kubwa za kufufua utaratibu wa amani kati ya wa-Israel na wa-Palestina juhudi ambazo zimelenga kwenye kubuni taifa tofauti la wa-Palestina pembeni ya Israel.

Lakini mazungumzo kati ya Israel na mamlaka ya wa-Palestina yalivunjika mwaka 2014. Tangu wakati huo kumekuwepo na ongezeko la ghasia kati ya wa-Palestina na wa-Israel.

XS
SM
MD
LG