Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:32

Marekani kwenye hatari ya kutolipa madeni yake


Rais wa Marekani Joe Biden kwenye ikulu ya Marekani Jumatatu.
Rais wa Marekani Joe Biden kwenye ikulu ya Marekani Jumatatu.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu amewashutumu vikali wabunge wa Republican kwa kuwazuia wabunge wa Democratic kuiruhusu serikali kuongeza kiwango cha kukopa pesa ili iweze kulipa madeni yake.

Kulingana na wizara ya fedha ya Marekani, tarehe 18 ya mwezi huu, nchi inaweza kuishiwa na fedha na hivyo kushindwa kulipa madeni yake, ikiwa bunge litashindwa kuafikiana kuhusu kuiwezesha serikali kukopa pesa.

Biden amesema hawezi kuhakikisha kwamba Marekani haitashindwa kulipa madeni yake kwa mara kwanza, akimtaka kiongozi wa Warepublican kwenye baraza la Seneti Mitch McConnel kuwaruhusu Maseneta wa chama cha Democrat kuongeza bila pingamizi kiwango cha kukopa ili kulipa deni la Marekani la dola trillioni 28.4.

Biden amesema iwapo serikali itashindwa kulipa madeni yake basi warepublican watawajibika kwa hilo.Watalaam wa masuala ya uchumi wanatabiri kuwa nchi kushindwa kulipa madeni itakua na athari mbaya kwenye soko la hisa la Marekani na kwenye uchumi wa dunia. Kuna

uwezekano pia hali hiyo itapelekea serikali kuchelewesha malipo ya pensheni kwa wamarekani wakongwe.

Jumatatu McConnel alituma barua kwenye ikulu ikisema kwamba warepublican hawako tayari kushirikiana na wademocrat kusuluhisha mzozo wa deni la nchi.

Naye kiongozi wa wademocrats katika Senate Chuck Schumer amesema wademocrat 50 katika baraza hilo lenye maseneta 100, watatumia mfumo wa kupata kura ya 51 ya makamu rais Kamala Harris ili kuupitisha mswaada wa kuiruhusu serikali kukopa pesa ili kulipia madeni yake.

XS
SM
MD
LG