Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:14

Marekani kuzindua kampeni dhidi ya uvutaji sigara


Taasisi ya udhibiti wa magonjwa Marekani ikionyesha sampuli ya tangazo jipya la kampeni ya kupambana na uvutaji sigara.
Taasisi ya udhibiti wa magonjwa Marekani ikionyesha sampuli ya tangazo jipya la kampeni ya kupambana na uvutaji sigara.

Kutokana na vifo vinavyotokana na magonjwa yanayohusiana na uvutaji serikali ya Marekani itazindua kampeni kali ya kuwashtua wavutaji.

Marekani imeanza juhudi mpya za kupunguza kiwango cha wavutaji sigara nchini kwa kutumia matangazo ya kibiashara yanayoonyesha sura za kushtua za watu waliopata madhara ya kudumu maishani kutokana na uvutaji sigara kwa miaka Idadi ya watu wazima wanaovuta sigara ilifikia asili mia 40 miaka ya 60 nchini Marekani na inazidi kuongezeka. Mamilioni ya watu hufa kila mwaka kutokana na magonjwa yanayohusiana na uvutaji sigara. Kutokana na hilo serikali ya Marekani imesema kuanzia Jumatatu ijayo itazindua kampeni kali ya dola milioni 54 kupitia matangazo ya kibiashara yanayolenga kuwashtua wavutaji sigara ili wakome kabisa kuvuta sigara na kuwazuia vijana kuvutiwa na tabia hiyo hatari kwa maisha yao. Taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya Marekani (CDC) itatumia matangazo hayo ya kibiashara kwenye radio, televisheni na mitandao ya kijamii pamoja na mabango katika muda wa miezi mitatu. Mfano wa tangazo mojawapo la kibiashara linaonyesha mwanamume wa miaka 31 ambaye amekatwa miguu yote miwili baada ya kupata ugonjwa unaoathiri damu na ambao husababishwa na uvutaji sigara. Tangazo hilo pia lina maandishi yanayosema, ‘jipe muda zaidi asubuhi kuvaa miguu yako.’ Matangazo mengine ya kibiashara yanaonyesha watu wenye mashimo makubwa shingoni na ambao walilazimika kufanya upasuaji kwa sababu ya saratani inayotokana na uvutaji sigara. Kampeni hiyo pia inazinduliwa wakati serikali ya Marekani inapambana vikali kisheria ikiyataka makampuni ya utengenezaji sigara yaweke onyo kali mbele na nyuma ya pakiti za sigara ikielezea bayana madhara yanayotokana na uvutaji sigara.

XS
SM
MD
LG