Mazungumzo hayo yatajumuisha Umoja wa Afrika, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu na Umoja wa Mataifa kama waangalizi, Blinken amesema katika taarifa yake.
Saudi Arabia itakuwa mwenyeji mwenza wa majadiliano hayo, aliongeza kusema. “Kiwango cha vifo, mateso na uharibifu nchini Sudan ni kibaya sana.
Mzozo huu usio na maana lazima umalizike,” Blinken amesema, akitoa wito kwa jeshi la Sudan, na vikosi vya akiba RSF, kuhudhuria mazungumzo.
Vita vya Sudan, vilizuka mwezi Aprili 2023, na vimewalazimu takribani watu milioni 10 kukimbia na kusababisha tahadhari ya njaa na ghasia za kikabila RSF ikilaumiwa kwa kiwango kikubwa.
Forum