Jopo la mahakama la mji wa kusini wa Tampa katika jimbo la Florida limedai kuwa mawakala wa usalama wa Russia walitoa mafunzo, kufadhili na kuyaelekeza makundi ya kisiasa ya Marekani wadai kuwa mawakala wa Moscow wasio sajiliwa, ili kueneza chuki na propaganda ya Russia.
Mashtaka hayo yanachukua nafasi ya yale ya hapo awali yaliyodai kwamba mawakala wa kijasusi wa Russia walifadhili na kusimamia kampeni za kisiasa za ofisi moja hapa Marekani.
Naibu mwanasheria mkuu katika wizara ya sheria ya Marekani kwenye kitengo cha usalama wa taifa, Matthew Olsen alisema katika taarifa kwamba majasusi wa Russia walitumia vibaya haki ya marekebisho ya kwanza ya katiba ya Marekani, ambayo serikali ya Russia inawanyima raia wake, kuwagawa wamarekani pamoja na kuingilia uchaguzi ndani ya Marekani.