Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 06:22

Marekani kuendelea kuinga mkono Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, nchini Ukraine.
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, nchini Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken yuko nchini Ukraine katika ziara ambayo ilikuwa haijatangazwa kuonyesha jinsi Washington inavyoendelea kuiunga mkono Kyiv, miezi sita baada ya uvamizi wa Russia nchini humo.

Blinken Alhamisi alitangaza msaada wa dola bilioni 2.6 kwa Ukraine na nchi nyingine 18 katika eneo “nchi nyingi ziko katika hatari ya kukabiliwa na uchokozi wa Russia siku za usoni.”

“Ni wakati hasa wa matukio kwa Ukraine” huku nchi hiyo hivi karibuni ikiwa imeadhimisha Siku ya Uhuru wake na huku wananchi wa Ukraine wakiwa “wamejikita kujibu mashambulizi” dhidi ya uvamizi wa kijeshi wa Russia, afisa wa ngazi ya juuu wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema.

Ziara ya Blinken huko Kyiv pia imefanyika kabla ya Mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo viongozi wa dunia wanajitayarisha kukusanyika kwa kile maafisa wa Marekani walichosema ni tukio la kuthibitisha misingi ya Mkataba wa UN juu ya uhuru na heshima ya maeneo.

“Tunajikita kusaidia kuhakikisha kuwa Ukraine inaendelea kuwepo katika vita hivi na tunatoa msaada wa kiusalama ili tukifika katika siku ambayo tutafanya mazungumzo ya usuluhishi, Ukraine itakuwa katika nafasi yenye nguvu,” afisa wa ngazi ya juu alisema.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin pia ametangaza Alhamisi kuwa Marekani inapanga kuipa Ukraine msaadampya wa kiusalama wenye thamani ya hadi dola milioni 675, wiki mbili baada ya Washington kuahidi dola bilioni 3 za fungu la msaada wa usalama kwa Kyiv.

Msaada huo wa ziada wa usalama utajumuisha silaha zaidi kama Howitzers, High Mobility Artillery Rocket Systems au HIMARS, makombora ya kujihami na miale ya nyuklia ya spidi ya juu, mashine za kufyatua mabomu, magari ya kivita ya huduma ya kwanza, vifaa vya kuonea usiku, ikiwa pamoja na vifaa vingine.

Misaada hiyo inafikisha idadi ya misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine kufikia takriban dola bilioni 15.2 tangu kuingia madarakani utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden

Austin alisema vita nchini Ukraine “viko katika wakati mwingine muhimu” wakati majeshi ya Ukraine yakiendelea kukabiliana na uvamizi wa Russia upande wa kusini wa nchi hiyo, na kuwa “hivi sasa tunaona mafanikio ya wazi ya juhudi zetu za pamoja katika uwanja wa vita.”

Pia alisema kikundi cha mawasiliano kitafanya kazi kwa pamoja kuyafundisha majeshi ya Ukraine na kuwapatia mahitaji ya Ukraine ya kijeshi “ katika safari hthank Sawa for the inii ngumu.”

“Ni lazima tubadilike kwa kadiri mapambano yanavyobadilika,” Austin alisema.

Siku ya Jumatano, mkuu wa majeshi ya Ukraine, Valeriy Zaluzhny, alisema wazi kwa mara ya kwanza kuwa Ukraine ilikuwa imefanya mashambulizi ya makombora ambayo yalipiga vituo kadhaa vya kijeshi vya Russia katika eneo linalokaliwa na Russia kwa mabavu huko Crimea, kulingana na shirika la habari la AFP.

Baadhi ya taarifa katika repoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG