Wakati ratiba ya pendekezo hilo inayotarajiwa kuchukuwa wiki kadhaa, bado haijatolewa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller amewaambia wanahabari Jumatatu kwamba Washington inafanya kazi kwa haraka kuhakikisha pendekezo hilo linaleta makubaliano ya mwisho kati ya Israel na Hamas.
Mapema Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alikutana na Yair Lapid, kiongozi wa upinzani wa Israel na waziri mkuu wa zamani.
Baada ya mkutano huo katika Wizara ya Mambo ya Nje, Lapid aliwaambia wanahabari kwamba Israel inataka makubaliano ya mateka na kusitisha vita, akisisitiza hakuna mchakato wa kisiasa au misukosuko inayopaswa kuathiri mpango huo.
Forum