Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 14:48

Marais wa Sudan na Sudan Kusini washtumiana


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir

Rais wa Sudan Kusini akanusha madai kwamba serikali yake inaunga mkono waasi.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amekanusha madai kutoka Khartoum kuwa serikali yake inaunga mkono waasi wanaopigana na majeshi ya serikali ya Sudan. Bwana Kiir pia ameshtumu rais wa Sudan Omar al-Bashir kwa kupanga njama za kushambulia nchini yake. Rais Kiir aliwaambia wandishi habari kuwa madai dhidi yake kwamba anaunga mkono waasi katika majimbo ya Blue Nile na South Kordofan ni ya uwongo na kwamba yamepangwa kumharibia sifa. Rais wa Sudan Omar al-Bashir anaishtumu Sudan Kusini kwamba inaunga mkono waasi was South Sudan People’s Liberation Movement-North (SPLM-N.) Kundi hilo lilikuwa la wapiganaji upande wa Sudan Kusini wakati nchi hiyo ikiwa moja. Rais huyo wa Sudan Kusini alikuwa akizungumza mjini Juba ambapo alisema madai ya bwana Bashir yaanashiria hatua katika siku zijazo. Bwana Kiir anasema ,“ukweli ambao watu hawasemi ni kwamba Bashir na kundi lake wanaamini kwamba walifanya makosa makubwa kuruhusu ardhi yetu inayopendeza na ambayo inaitwa Sudan Kusini kumilikiwa na kile wanaochoita makafiri au watu wasiomcha Mungu, na kwamba ni sharti wainyakue tena.” Matamshi ya Rais Kiir yalitolewa baada ya Rais wa Sudan Omar al-Bashir kutishia kurejea vitani na Sudan Kusini. Alinukuliwa mapema wiki hii katika gazeti la Sudan Tribune akisema ikiwa Sudan Kusini inataka vita jeshi lake lipo tayari.

XS
SM
MD
LG