Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 12:33

Marais wa Kenya na Sudan wajadiliana kuhusu biashara na usalama


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika picha
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika picha

Mkutano wa kwanza ulikuwa wa ana kwa ana baina ya marais hao wawili na wa pili ulihudhuriwa pia na ujumbe wote wa marais.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Sudan Omar Hassan al Bashir Jumamosi walifanya mazungumzo ya pande mbili katika makazi ya rais mjini Khartoum ambapo agenda muhimu ilikuwa masuala ya usalama na biashara.

Rais Kenyatta aliyoko nchini humo katika ziara ya siku mbili alifanya mikutano miwili na rais Bashir.

Mkutano wa kwanza ulikuwa wa ana kwa ana baina ya marais hao wawili na wa pili ulihudhuriwa pia na ujumbe wote wa marais.

Katika mkutano huo viongozi hao walijadili kuhusu kuongeza juhudi ili kusaidia katika kuleta uthabiti nchini Sudan kusini na Somalia.

Wote Kenya na Sudan wanahifadhi wakimbizi kutoka sudan kusini na Somalia na marais hao wawili wamesema ni jambo muhimu kuhakikisha uthabiti unakuwepo katika nchi hizo.

Pia wamekubaliana kupanua wigo wa biashara ambapo rais Kenyatta wa Kenya amesema nchi yake inakaribisha wananchi wa Sudan kutafuta fursa zaidi katika sekta za utalii , fedha na uwekezaji.

XS
SM
MD
LG