Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:05

Marais Putin na Kim wakutana huku Marekani na Korea Kusini wakitoa onyo


Rais wa Russia, Vladimir Putin, Jumatano amekutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un katika kituo cha Russia, ambacho kimeendelea zaidi katika teknolonojia ya mambo ya anga katikati ya tahadhari za Marekani na Korea Kusini kupinga makubaliano yoyote ya silah

Rais Kim, aliahidi msaada kamili usio na masharti yoyote kwa maamuzi ya Rais Putin, ambapo kwa hakika alikuwa akizungumzia vita vya Russia, na Ukraine, wakati viongozi hao wawili walipofanya mazungumzo katika eneo la Vostochny Cosmodrone lililopo katika mkoa wa Russia, Amur, uliopo mashariki ya mbali karibu na mpaka na China.

Mkutano umefanyika wakati taarifa za vyombo vya habari zikinukuu maafisa wa mataifa ya magharibi wakisema Russia, inatarajia kupokea silaha kutoka Korea Kaskazini, na kuzitumia katika vita dhidi ya Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG