Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:28

Mapigano yazuka tena Sudan siku moja baada ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano


Moshi waonekana nyuma ya majengo kusini mwa Khartoum, Mei 27, 2023, huku mapigano yakiendelea kati ya majeshi ya majenerali wawili hasimu
Moshi waonekana nyuma ya majengo kusini mwa Khartoum, Mei 27, 2023, huku mapigano yakiendelea kati ya majeshi ya majenerali wawili hasimu

Mapigano yamezuka tena Jumanne nchini Sudan licha ya ahadi za hivi karibuni za Majenerali wawili hasimu kusitisha mapigamo ili kuruhusu misaada inayohitajika sana kuwafikia raia waliozingirwa.

Jeshi la Sudan na kikosi cha Rapid Support Forces walikubaliana rasmi jana Jumatatu kuongeza kwa siku tano za sitisho la mapigano kwa ajili ya usambazaji wa misaada ya kibinadamu, sitisho hilo limefikiwa chini ya upatinishi wa Marekani na Saudi Arabia, lakini lilikiukwa mara kwa mara wiki iliyopita.

Tangu muda wa kusitisha mapigano kuongezwa, mapigano zaidi yaliripotiwa na wakazi, yakiwemo mapigano kwa kutumia aina mbalimbali za silaha kusini mwa Khartoum, na mapigano katika jimbo la Nyala la Darfur Kusini.

Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa kikosi cha RSF Mohammed Hamdan Dagalo, kwa mara nyingine wamelaumiana kukiuka makubaliano hayo na kudai kwamba wamejibu uchokozi wa adui.

Vita hivyo vimeua watu 1,800, na zaidi ya watu milioni 1 wamelazimika kuhama makazi yao na karibu watu 350,000 walikimbilia katika nchi jirani, Umoja wa Mataifa umesema.

Forum

XS
SM
MD
LG