Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 16:05

Mapigano yamemalizika Sudan na Sudan Kusini.


Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir akizungumza na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.

Vikosi vya Sudan na Sudan Kusini vyaripotiwa kuondoka mpakani kuashiria kumalizika kwa mapigano hayo.

Mapigano hatimaye yamemalizika kwenye mpaka wa Sudan na Sudan Kusini ambapo mashambulizi ya anga na ardhi yalifanyika wiki hii.

Mpaka Alhamisi asubuhi vikosi viliripotiwa kuondoka kwenye pande zote za mpaka. Lakini kungali na idadi ndogo ya wanajeshi,vifaru na magari makubwa kwenye eneo la Heglig ikiwa ni ushahidi wa vita vilivyotokea.

Mapigano hayo yanamefanywa siku kadhaa kabla ya mkutano wa marais wa Sudan na Sudan Kusini uliotegemewa kuzungumzia mafao ya mafuta na mipaka. Rais wa Sudan Omar al-Bashir amesema anasitisha mkutano huo wa Aprili 3 na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa sababu ya ghasia hizo.

XS
SM
MD
LG