Silaha nzito na bunduki za rashasha zilisikika zikifyatuliwa alfajiri karibu na mashariki mwa Deir al-Balah katika video iliyochukuliwa na The Associated Press, huku mitaa ikiwa haina watu.
Katika mji wa kusini wa Khan Younis, watu wanne waliuawa katika shambulizi la mapema la Israel dhidi ya gari lao, alisema msemaji wa Ulinzi wa Raia wa Palestina Mahmoud Bassal.
Bassal aliripoti Alhamisi usiku kwamba watu 24 waliuawa siku moja kabla katika mashambulizi kadhaa kote Ukanda wa Gaza na jeshi la Israeli, pamoja na Gaza City upande wa kaskazini na Khan Younis upande wa Kusini.
Alisema mashambulizi hayo pia yalisababisha majeruhi wengi lakini hakueleza ni wangapi.
Forum