Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:04

Mapigano yaendelea Syria


Saa chache baada ya maafisa wa Russia na Syria kuthibitisha wameongeza muda wa kusimamishwa kwa mapigano mjini Aleppo, wanasiasa wa upinzani wamesema ndege za kivita za serekali ya Syria ama Russia zilifanya mashambulizi.

Mashambulizi makali yalifanyika kilometa 30 kutoka katika mji ambao umewahi kuwa mji mkuu wa kibiashara katika kambi ya wakimbizi karibu na mpaka wake na Uturuki.

Karibu watu 30 waliuwawa katika kambi ya Kamouna karibu na Satmada kaskazini mwa jimbo la Syria, Idlib.

Darzeni ya watu walijeruhiwa kwa mujibu wa kamati ya huko ya uratibu LCC, ambayo ni mtandao wa shughuli za kumpinga Rais Assad.

Kundi lingine la wanaharakati lenye makao yake Uingereza Syrian Observatory for Human Rights limesema idadi ya watu waliokufa ni 28, ikijumuisha wanawake, watoto lakini ikaonya kuongezeka kwa idadi ya vifo.

XS
SM
MD
LG