Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 03:50

Mapigano yaendelea Sudan Kusini


Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini Desemba 16, 2013
Mapigano ya risasi yamezuka upya leo katika mji wa Juba mji mkuu wa Sudan Kusini, siku moja baada ya rais Salva Kiir kusema serikali imefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi na kwmaba inadhibiti mji huo.

Mapigano yalianza Jumapili usiku na kuendelea jana Jumatatu na leo Jumanne huko Juba huku maafisa wakisema yamesababisha vifo vya watu 26 na kujeruhi zaidi ya mia moja.

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo inakisia kuwa zaidi ya watu laki moja wametafuta hifadhi kwenye viwanja vyake viwili mjini humo na 39 wamelazwa hospitali kwa matibabu.
Hilde Johnson, mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo , amewasihi viongozi wa Sudan Kusini kujizuia kuchukua hatua ambazo zitachochea hali ya mvutano zaidi.

Bw. Kiir jana alisema mapigano yalianza pale wanajeshi watiifu kwa makamu rais wa zamani Riek Machar waliposhambulia makao makuu ya kijeshi. Machar alifutwa kazi mwezi Julai.
XS
SM
MD
LG