Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:25

Mapigano mapya yamezuka DRC - Mashahidi


Wanajeshi wa serikali ya DRC wapigana na waasi wa M23 karibu na mji wa Rutshuru.
Wanajeshi wa serikali ya DRC wapigana na waasi wa M23 karibu na mji wa Rutshuru.

Mapigano yalianza tena Jumatano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya wanajeshi na kundi lenye silaha la M23, wakaazi wameliambia shirika la habari la AFP, siku moja baada ya idadi kubwa ya watu kukimbia maeneo yanayodhibitiwa na waasi yalipokuwa yakishambuliwa na ndege za kijeshi.

Wakazi waliiambia AFP kuwa walikuwa wamesikia sauti za mapigano zaidi kufikia jioni, baada ya siku yenye wasiwasi lakini tulivu.

"Kuna milipuko ya mabomu. Jeshi linapiga maeneo ya M23," alisema mkazi mmoja wa kijiji nje ya kitovu cha kibiashara cha Rugari.

Waandishi wa habari wa AFP mjini Goma waliona ndege mbili za kivita na helikopta mbili zikiruka juu Jumatano.

Maafisa walisema Jumanne kwamba jeshi la DRC lilitumia ndege mpya zilizotumwa kushambulia maeneo ya M23 mashariki mwa nchi, huku baadhi ya wakaazi wakikimbia kuvuka mpaka.

Kundi linaloundwa na Watutsi wengi wa Kongo, M23 lilijipatia umaarufu kwa mara ya kwanza mwaka 2012 – na kwa muda mfupi liliteka jiji kuu la mashariki mwa DRC, Goma, kabla ya kufurushwa.

Umoja wa Mataifa ulisema Jumatano kwamba takriban watu 188,000 wamekimbia vijiji vyao tangu Oktoba 20, mwanzo wa mashambulizi mapya ya M23. Takriban 16,500 wamekimbilia nchi jirani ya Uganda.

XS
SM
MD
LG