Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wanaripoti kutokea mapigano makubwa kaskazini mwa mji wa Aleppo ambako vikosi vya serikali vimekuwa vikipigana na waasi ambao wanajaribu kuchukua udhibiti wa mji huo wa kibiashara.
Wanaharakati wanasema mapigano makubwa yanaendelea Jumanne katika maeneo jirani na watu 15 wamefariki dunia wakati vikosi vya usalama vikizima ghasia katika jela kwenye mji huo .Kamati ya ndani ya upinzani imesema vikosi vya usalama vya serikali pia vilipiga makombora katika maeneo nje ya Damascuss Jumanne pamoja na miji mingine ya Deir Ezzor na Homs.
Hapa Marekani Rais Baraka Obama ameungana na viongozi wengine wa dunia kuionya Syria kutumia silaha za kemikali. Bwana Obama alisema Bwana Assad atawajibishwa kama Syria itatumia gesi ya sumu au kemikali nyingine za mauaji.
Mapigano makubwa yaripotiwa katika mji wa Aleppo ambapo watu 15 wafariki dunia.