Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:59

Mapigano makali yazuka kati ya makundi hasimu ya chama cha Riek Machar


 Makamu Rais wa Sudan Kusini Riek Machar
Makamu Rais wa Sudan Kusini Riek Machar

Mapigano makali yalizuka Jumamosi kati ya makundi hasimu ya Makamu Rais wa Sudan Kusini Riek Machar cha SPLA-IO, msemaji wake wa jeshi amesema katika taarifa.

Mapigano makali yalizuka Jumamosi kati ya makundi hasimu ya Makamu Rais wa Sudan Kusini Riek Machar cha SPLA-IO, msemaji wake wa jeshi amesema katika taarifa.

Mapambano yalizuka baada ya mahasimu wa Machar kutangaza wiki hii kuwa wamemuondoa kama mkuu wa chama na kwenye uongozi wa kijeshi wa chama hicho.

Majeshi yalikuwa yakiongozwa na jenerali hasimu katika chama, Simon Gatwech Dual, ambaye alianzisha shambulizi kwa watu wa Machar, ambao “walichukizwa na wachokozi,” msemaji Col. Lam Paul Gabrie amesema.

Jeshi la Machar la SPLA-IO limewaua mameja jenerali wawili na wengine zaidi ya 27 “wanajeshi adui” wakati wao wamepoteza watu watatu tu, aliongezea.

Mapigano hayakuwezwa kuthibitishwa na vyanzo huru na hakuna majibu ya haraka kutoka upande wa Gatwech Dual.

Viongozi wa tawi la kijeshi la Machar la SPLM/A-IO wamesema Jumatano kuwa walimuondoa kiongozi ambaye aliwahi kuwa muasi na hivi sasa ni mwanasiasa kwa kushindwa kuwakilisha maslahi yao.

Mapigano yanaweza kuweka shinikizo kwa makubaliano tete ya mwakao 2018 ya kushirikiana madarakani kati ya Machar na hasimu wake wa zamani Rais Salva Kiir.

Washirika wa Machari, Ijumaa walitupilia mbali kuondolewa kwake madarakani na kusema kuwa ni “mapinduzi yaliyofeli” na kusisitiza kuwa bado ana udhibiti kamili katika chama.

Machar mwenyewe wiki hii aliwashutumu “waharibifu wa amani” kwa kufanya njama za kumuondoa mamlakani.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 68 amenusurika katika miaka kadhaa ya vita vya msituni, majaribio ya kuuawa na kuishi muda mrefu uhamishoni, amehudumu kama makamu rais pamoja na Kiir katika serikali ya kwanza baada ya uhuru kutoka Sudan mwaka 2011.

Viongozi hao wawili baadaye walikosana, na Machar alifukuzwa kazi miaka miwili baadaye. Wanajeshi watiifu kwa kila upande walishikiana silaha, na Sudan Kusini ilitumbukia katika miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

XS
SM
MD
LG