Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 15:38

Mapigano makali na maafa yaripotiwa Kinshasa


Majeshi ya DRC yadhibiti makao makuu ya televisheni mjini Kinshasa. Dec. 30, 2013
Majeshi ya DRC yadhibiti makao makuu ya televisheni mjini Kinshasa. Dec. 30, 2013
Maafisa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanasema majeshi ya serikali yamedhibiti maeneo matatu katika mji mkuu wa Kinshasa na kuuwa washambuliaji 40 na kuwakamata wengine wengi.

Msemaji wa serikali Lambert Mende amesema magenge ya watu waliojihami walishambulia uwanja wa kimataifa wa ndege leo jumatatu ikiwa ni pamoja na kituo cha kitaifa cha televisheni na makao makuu ya jeshi mjini Kinshasa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:04 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Amesema baadhi ya washambuliaji wameuawa katika maeneo yote matatu. Aidha Mende anawaelezea washambuliaji hao kuwa ‘magaidi’ lakini anasema hawajatambulishwa.

Anasema washambuliaji hao hawakuonekeana kuwa na lengo maalum ila kuvuruga sherehe za kukaribisha mwaka mpya.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Kinshasa alisema kuwa milio ya risasi ya hapa na pale imesikka wakati wa mchana na wakazi wengi wamebaki manyumbani mwao.
Anasema polisi na wanajeshi wanapiga doria kote mjini humo na wameweka vituo vya ukaguzi.

Nao ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa umewashauri wamarekani kuepuka maeneo yenye mikusanyiko ya umati wa watu.
XS
SM
MD
LG