Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Jean-Pierre Bemba, ambaye alikuwa gerezani kwa zaidi ya miaka 10 kwa uhalifu wa kivita, kuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo katika mabadiliko makubwa kwenye serikali. Uteuzi wake ulikuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya maafisa 57 wa serikali, ambayo msemaji wa rais alisema ni ya "haraka na lazima", katika tangazo kupitia kituo cha televisheni ya taifa ya Kongo. Rais huyo pia amemteua Vital Kamerhe, mkuu wake wa zamani wa utawala, ambaye aliachiliwa kutoka gerezani mwezi Desemba 2021 baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu, wakati alipokuwa waziri wa Fedha. Kamerhe Juni mwaka 2022 alifutiwa mashtaka yote baada ya kukataa rufaa dhidi ya mashtaka hayo. Mabadiliko hayo, ambayo yalikuwa makubwa zaidi kuliko ilivyotabiriwa, yamekuja kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Desemba 20, ambapo Tshisekedi anatarajiwa kuwania muhula wa pili.
Maoni ya raia wa DRC kuhusu uteuzi wa Bemba na Kamerhe kuwa mawaziri
Matukio
-
Machi 14, 2025Changamoto za ulezi wa watoto walemavu kiakili Kenya
-
Februari 28, 2025Waislamu wajitayarish kwa Ramadhani
-
Februari 27, 2025Ethiopia na Somalia waimarisha uhusiano wao
-
Februari 18, 2025Nini kilichosababisha Raila Odinga kushindwa katika uchaguzi wa AU?
-
Februari 11, 2025Naibu Katibu Mkuu aeleza hatua za dharura zinazochukuliwa DRC