Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:15

Manahodha Mombasa kufunguliwa mashtaka


Aina ya boti ya kuvulia samaki
Aina ya boti ya kuvulia samaki

Manahodha hao tayari wamehojiwa kwa siku moja, kabla ya polisi kuwapa dhamana ya takriban dola elfu tano kila mmoja, huku wakisubiri mashtaka rasmi.

Wakuu wa polisi kisiwani Lamu, Mombasa , Kenya wanapanga kuwafungulia mashtaka manahodha wa mashua mbili zilizogongana usiku wa sherehe za mwaka mpya, na kupelekea mauti takriban watu 10.

Manahodha hao tayari wamehojiwa kwa siku moja, kabla ya polisi kuwapa dhamana ya takriban dola elfu tano kila mmoja, huku wakisubiri mashtaka rasmi.

Japo ripoti ya polisi inasema watu 9 pekee walikufa katika mkasa huo baharini, kuna hofu huenda zaidi ya watu 20 waliangamia Jumapili usiku.

Mkuu wa mkoa wa pwani Earnest Munyi ambaye ametembelea eneo la mkasa, anasema hamna matumaini ya kuwapata manusura zaidi.

Takwimu kutoka Red Cross zinaonyesha kwamba kufikia Jumatano asubuhi miili iliyopatikana ni ya watu 9, waliookolewa ni watu 25, wale walioogelea wenyewe na kujinusuru ni watu 23, na kufikia sasa watu 16 wametoweka baharini.

Mwenyekiti wa Kenya Red Cross tawi la Mombasa Abdallah Miraj ameviambia vyombo vya habari kuwa kuna uwezekano mashua hiyo ilikuwa na abiria 82, waliokuwa wanavuka ili kusafiri kwa mabasi kutoka Lamu kisiwani.


XS
SM
MD
LG