Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:30

Mamlaka za Russia zinavunja mifumo ya huduma ya afya Ukraine


Ghasia zinazoendelea katika mji wa Kherson nchini Ukraine
Ghasia zinazoendelea katika mji wa Kherson nchini Ukraine

"Wavamizi wameamua kufunga taasisi za matibabu katika miji, kuchukua vifaa, magari ya kubeba wagonjwa - kila kitu tu. Wanaweka shinikizo kwa madaktari ambao bado wako  katika maeneo yanayokaliwa kimabavu ili wahamie katika eneo la Russia," Rais Zelenskyy alisema.

Mamlaka za Russia katika maeneo wanayoyakalia kimabavu ya Ukraine zinavunja mifumo ya huduma za afya za mikoa hiyo, rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku Ijumaa.

"Wavamizi wameamua kufunga taasisi za matibabu katika miji, kuchukua vifaa, magari ya kubeba wagonjwa - kila kitu tu. Wanaweka shinikizo kwa madaktari ambao bado wako katika maeneo yanayokaliwa kimabavu ili wahamie katika eneo la Russia," rais alisema.

"Russia inaugeuza mkoa wa Kherson kuwa eneo lisilo na ustaarabu, bila vitu vya msingi vinavyopatikana katika nchi nyingi duniani," alisema Zelenskyy. "Kabla ya kuwasili kwa Russia, mkoa huu, kama ilivyo mikoa mingine yote ya Ukraine, ulikuwa wa kawaida kabisa na salama, huduma zote za kijamii kwa watu zilihakikishiwa huko. Maisha yalihakikishiwa huko."

"Na sasa Russia inajaribu kuufanya mkoa wa Kherson kuwa eneo likilotengwa," rais alisema. "Dunia lazima ichukue hatua kwa hili."

Mkoa wa Kherson pia ulikuwa lengo la ripoti za ziada za kijasusi za Wizara ya Ulinzi ya Uingereza Jumamosi. Ripoti hiyo ilisema mapema wiki hii, Vladimir Saldo, gavana aliyeteuliwa na Russia kwa mkoa wa Kherson, alidai kuwa zaidi ya watu 70,000 waliondoka katika mji wa Kherson.

XS
SM
MD
LG