Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa alisema Jumanne kwamba Mamlaka ya Palestina inaweza kuomba uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa mwaka huu. “Huu ni uwekezaji katika amani na uwekezaji katika suluhisho la mataifa mawili”, Balozi Riyad Mansour aliwaambia waandishi wa habari katika Umoja wa Mataifa.
Mnamo Novemba 2012, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipiga kura ya kupandisha hadhi ya Wa-palestina ya kuwa mwangalizi asiye mwanachama, na kumruhusu balozi wake kushiriki katika mijadala na mashirika ya Umoja wa Mataifa lakini bila kupiga kura.
Palestine Liberation Organization ilitambuliwa kama muangalizi tu mwaka 1974. Mansour anasema Mamlaka ya Palestina, kwa uungaji mkono na mataifa ya Kiarabu, itaanza kuhamasisha msaada kwenda kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo linashikilia funguo ya uanachama kwa sababu ni lazima iunge mkono ombi kabla ya kwenda kwenye Baraza Kuu kwa uamuzi wa mwisho.
Hii ina maana kwamba angalau wajumbe tisa wa baraza hilo lazima wapige kura kuunga mkono hatua hiyo, na hakuna hata mmoja kati ya wanachama watano wa kudumu anayeweza kutumia kura ya turufu.
Forum